MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA
Habari yenu wapenzi wasomaji wa blog mahususi kwa masuala ya kilimo na ufugaji, ni matumaini yangu kuwa hamjambo na mnendelea vema kusukuma gurudumu hili zito la kulijenga taifa letu Leo nawaletea makala hii ili tuweze kujua matumizi sahihi ya mbolea ktk kilimo chetu, kwani kilimo ni sekta muhimu katika taifa letu Somo la mbolea Yara Tanzania Ltd ni kampuni inayojiusisha na utengenezaji, usambazaji, uuzaji na utoa elimu kuhusu Mbolea za mazao mbalimbali. Mbolea katika maana nyepesi ni Lishe ya mmea. Hivyo huwa na viini lishe ambavyo ni muhimu ktk ukuaji, uotaji, uzalishaji na ulinzi wa ubora mmea. Aina za mbolea 1- Mbolea za asiri(organic) mf. Samadi, Mboji n.k 2-Mbolea za viwandani(Inorganic) DAP, Winner, Tsp, SA, n.k Mbolea za viwandan pia naweza kuzigawa kat...