DHANA YA KAMUSI
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
CHUO CHA UALIMU CHA MT. MAURUS
MADA NDOGO :KAMUSI YA LUGHA
MWALIMU WA SOMO:LAMECK
MASAWALI
Nini maana ya kamusi?
Umuhimu wa kamusi
Mambo ya kuzingatia katika kamusi
Sifa za kamusi kubwa na kamusi ndogo
WASHIRIKI
Masal Masal
James Kalua
KAMUSI YA LUGHA; MAANA, AINA, TAARIFA NA DHIMA ZAKE.
MAANA YA KAMUSI
Massamba (2012:24) kamusi ni kitabu cha orodha ya maneno katika lugha, yaliyopangwa kwa utaratibu maalum, pamoja na maana au fasili zake; katika uchanganuzi wa lugha haya ni maneno ya kileksika, yaani yasiyokuwa ya kisarufi au kifonolija.
Tuki (1990:21) kamusi ni kitabu cha orodha ya maneno yaliyopangwa kwa utaratibu maalum, pamoja na maana na fasili zake.
Wamitila (2003:76) kamusi ni kitabu ambacho kina orodha ya maneno katika lugha Fulani ana ambayo hupangwa ki-abjadi au kialfabeti. Maneno haya huelezewa maana zake mbalimbali na labda hata vyanzo vyake.
Matinde (2012:273) kamusi ni kitabu chenye mkusanyiko wa maneno sanifu katika lugha mahususi yaliyoorodheshwa kialfabeti na kutoa taarifa za kifonetiki, kifonolojia, kimofolojia, kisintaksia, na hata kisemantiki.
Nyambari na Masebo (2012:179) kamusi ni kitabu cha marejeleo chenye msamiati uliokusanywa kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani, na kupangwa kwa utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo msomsji huweza kuelewa.
Kwa ujumla kamusi ni kitabu chenye orodha ya maneno mbalimbali yaliyopangwa vizuri kwa kufuata alfabeti na hutoa taarifa mbalimbali kama vile maana, matamshi n.k.
MUUNDO WA KAMUSI
i) Utangulizi wa Kamusi
Hii ni sehemu ya mwanzo ambayo hutangulia matini yenyewe ya kamusi.
ii) Matini ya Kamusi
Hii ni sehemu ambayo inaonyesha vidahizo na fahiwa zake kuanzia herufi A-Z.
iii) Sherehe ya Kamusi
hizi ni baadhi ya taarifa ambazo huwa zimeandikwa mwishoni mwa kamusi. Kwa mfano majina ya nchi, lugha za mataifa duniani, vipimo vya urefu, vipimo vya uzito, ujazo n.k.
AINA ZA KAMUSI
Kwa kutumia kigezo cha LUGHA kuna aina kuu tatu (3) za kamusi
i) kamusi wahidiya
hii ni kamusi inayoandikwa kwa lugha moja
ii) kamusi thaniya
Hii ni kamusi inayoandikwa kwa lugha mbili.
iii) kamusi mahuluti
Hii ni kamusi inayoandikwa kwa lugha zaidi ya mbili. Kwa mfano Kiswahili-kiingereza-kifaransa.
KWA KUTUMIA KIGEZO CHA UKUBWA
Zipo aina tatu za kamusi kwa kutumia kigezo hiki cha ukubwa kama ifuatavyo
(i)Kamusi ndogo-hii ni kamusi ambayo huwa na maneno yasiyozidi 10,000
(iiKamusi ya kati - hii ni kamusi ambayo huwa na maneno yasiyozidi 25,000
(iii)Kamusi kubwa- hii ni kamusi ambayo huwa na maneno zaidi ya 50,000
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KAMUSI
Kulingana na Newell (1995) amebainisha nduni zifuatazo za Kongoo
a. Maumbo yasiyo na mnyambuo ambayo hutokea katika hali ya Kifonolojia (Matamshi) ndiyo huingizwa katika kamusi mfano; mama, shangazi, sana, suri n.k
b. Maneno ambayo hayana viambishi ndiyo hudondolewa katika kamusi mfano; adhimisha, piga, adhimu vinaweza kuwa kidahizo.
c. Maumbo huru yenye sifa za kifofonemiki huweza kuorodheshwa kama kidahizo. Umbo lenye mkazo mmoja tu.
d. Maumbo yanayotambuliwa na wazungumzaji asilia wa lugha hiyo kama neno, yanaweza pia kuingizwa katika kamusi kama kidahizo. Hapa ni muhimu kupata tajiriba kutoka kutoka kwa wazawa.
e. Maumbo ambayo ni rahisi kuyabainisha kama neno yanapokuwa katika sentensi, huingizwa katika kamusi kama kidahizo:Kijana mdogo sana amesafiri leo asubuhi kwa ndege ya fastjet
f. Maumbo yanayotokea mara kwa mara mfano mtoto Vs Kitoto hutumika mara kwa mara katika maandishi na mazungumzo. Katika kongoo ya Kiswahili kuna maneno yapatayo milioni kumi (10,000,000/=).
g. Maumbo yote yale yanayowakilisha maana ya msingi (Basic meaning) ya leksimu huingizwa katika kamusi kama kidahizo mf. Askarikanzu, mpigambizi, amevaa miwani n.k
h. Maumbo ya mashina ambayo maneno nyambulishi mengine yanaweza kuundwa, yanaweza kuorodheshwa pia kama kidahizo
i. Maumbo yanayoweza kutumika kupata vitomeo vidogo (sub-entry) yanaweza kuingizwa katika kamusi kama kidahizo.
Mambo ya kuzingatia katika Uteuzi wa Vidahizo vya kamusi
1. Umbo la neno: ni lile umbo ambalo mtumiaji wa kamusi anatarajiwa kulitafuta, mfano: pig.a, stahimili, dada, askari (askarikanzu).
2. Muundo wa neno: neno linaweza kuundwa na:
- Mofimu huru moja mf. Kalamu, Nyoka, Baba na mama
- Mofimu zaidi ya moja kwa pamoja mf. Mchezaji (m-chez-a-ji), mkulima (m-ku-lim-a) n.k
- Maneno mawili au zaidi ambayo yameambatana na kuwa na maana moja mf. Kifungua kinywa (kifunguakinywa), mwana mapinduzi (mwanamapinduzi), askari kanzu (askarikanzu).
- Nahau, nahau ina hadhi ya neno kwa hiyo nayo inaingizwa katika kamusi kama kidahizo mf. Piga maji, vaa miwani, zunguka mbuyu.
3. Uingizaji wa viambishi:wasomaji wa kamusi hawatafuti viambishi, hata hivyo husaidia kuelewa maana zalishwa. Vioneshwe mbele ya shina la neno husika kwa kutenganishwa na alama ya mawimbi. Mf. To.a ~ le, ~lew,~an, ~lesh n.k
4. Tahajia: ni muhimu kufanya uamuzi wa tahajia itakayotumika kwa maneno yenye tahajia zaidi ya moja, kwa mf. Tasinifu Vs Tasnifu, Theatre Vs Theater, Burangeti Vs Blanketi, Kula Vs Kura
5. Majina ya Pekee: majina ya pekee huwa hayaingizwi katika kamusi kama kidahizo isipokuwa kwa yale ambaya yanahusishwa na uvumbuzi au mwanafalsafa fulani mf. Umaksi, Kanuni ya Newton. Maneno haya lazima yaingizwe katika kamusi kama kidahizo kutokana na sifa za ziadi yaliyonazo yanaondoka kuwa majina ya pekee tu.
6. Uingizaji wa Maneno ya Mkopo: tahajia ya maneno ya mkopo iingizwe kwa kufuata tahajia ya lugha lengwa. Mfano Editor – Edita – Editori, radio- redio- radio, machine-mashini – mashine. Baada ya kuwa mtunga kamusi umeamua ni tahajia ipi itatumika, chagua moja na itumike kwa kamusi nzima.
Taaarifa zinazopatikana katika kamusi
Taarifa hizi huweza kuwa za kisarufi au kileksika
a) taarifa za kisarufi zinazoingizwa katika kamusi.
Nyambari na Masebo (2012:184) wameainisha taarifa zifutazo za kisarufi zinazopatikana katika kamusi.
· Wingi wa nomino
· Kategoria ya kisarufi ya kidahizo mf. Kitenzi (kt), nomino (nm) n.k
· Vinyumbuo vya vitenzi mf. Piga-pigwa-pigana-pigika n.k
· Ngeli za nomino mf. Mtu (A-YU), kazi (i-)
· Matamshi ya neno
· Elekezi au sielekezi. Mfano: Apiza kt [ele], Anguka kt [sie]
· Mifano ya matumizi
b) Taarifa za kileksia zinazopatikana katika kamusi
Matinde (2012:275-281) anaeleza taarifa zifuatazo za kileksia ambazo zinapatikana katika kamusi ya lugha.
· Mpangilio wa vidahizo
· Kategoria za maneno
· Umoja na wingi
· Upatanisho wa kisarufi
· Uelekezi wa vitenzi
· Maana ya vidahizo
· Tahajia za maneno
· Mifano ya matumizi
· Methali, nahau na misemo
· Timolojia ya leksimu
· Michoro/ picha
· Matamshi
DHIMA ZA KAMUSI
· Huonesha tahajia sahihi za maneno
· Huonesha maana za maneno
· Huonesha matamshi sahihi ya maneno
· Huonesha asili ya neno
· Humsaidia mtumiaji kujifunza lugha za kigeni
· Huonesha alama na vifupisho mbalimbali katika lugha husika.
Marejeleo
Massamba. D.P.B.(2004 ). Kamusi ya isimu na falsafa ya lugha. Dares salaam: TUKI
Masebo . J. A. & Nyangwine. N. (2012). Kiswahili kidato cha tatu na nne . Dares salaam: nyambari nyangwine publishers
Matinde. R. S. (2012). Dafina ya lugha. Isimu na nadharia. Kwa sekondari, vyuo va kati na vyuo vikuu. Mwanza : Serengeti bookshop.
TUKI (1990).kamusi sanifu ya isimu na lugha. Dares salaam: Tuki na Educational publishers and distributors ltd.
Wamitila. K. W. (2003). Kamusi ya fasihi, istilahi na nadharia. Nairobi: Focus publishers ltd
Chomboz.blogspot.com(25/11/2018 16:20).Mambo ya kuzingatia katika kamusi
http://swa.gafkosoft.com(25/11/2018,16:21). Aina za kamusi
Dhana Ya Kamusi >>>>> Download Now
ReplyDelete>>>>> Download Full
Dhana Ya Kamusi >>>>> Download LINK
>>>>> Download Now
Dhana Ya Kamusi >>>>> Download Full
>>>>> Download LINK JA