KILIMO CHA UMWAGILIAJI (BUSTANI)
Habari wapendwa wasomaji wa ukurasa huu, natumaini mu wazima wa afya njema popote pale mlipo, lakini pia ningependa kutumia nafasi hii kuwakumbusha wasomaji wangu kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huu wa COVID-19 kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya. Leo napendaa kujadili juu ya kilimo cha umwagiliaji (bustani), kilimo hiki ni moja ya kilimo cha muda mfupi na kinacholipa zaidi kama utaweza kuzingatia vyema kwani hukua takribani miezi mitatu mpka minne Ili kilimo hiki kiwe chenye manufaa kwako yakupasa ufuate baadhi ya taratibu ambazo tutazijadili katika uzi huu, ili uweze kujikwamua na umasikini kwa kupitia aina hii ya kilimo yakupasa ufanye yafuatayo Tafuta eneo ambalo eneo ambalo upatikanaji wa maji ni wa mwaka mzima , yaani mwaka mzima maji hayakati labda kupungua tu. Hii itarahisisha /itakurahisishia wewe mkulima wa kilimo hiki katika harakati za umwagiliaji na kufanya mazao yako yawe yenye afya na bor...