KILIMO CHA UMWAGILIAJI (BUSTANI)
Habari wapendwa wasomaji wa ukurasa huu, natumaini mu wazima wa afya njema popote pale mlipo, lakini pia ningependa kutumia nafasi hii kuwakumbusha wasomaji wangu kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huu wa COVID-19 kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya.
Leo napendaa kujadili juu ya kilimo cha umwagiliaji (bustani), kilimo hiki ni moja ya kilimo cha muda mfupi na kinacholipa zaidi kama utaweza kuzingatia vyema kwani hukua takribani miezi mitatu mpka minne
Ili kilimo hiki kiwe chenye manufaa kwako yakupasa ufuate baadhi ya taratibu ambazo tutazijadili katika uzi huu, ili uweze kujikwamua na umasikini kwa kupitia aina hii ya kilimo yakupasa ufanye yafuatayo
Tafuta eneo ambalo eneo ambalo upatikanaji wa maji ni wa mwaka mzima, yaani mwaka mzima maji hayakati labda kupungua tu. Hii itarahisisha /itakurahisishia wewe mkulima wa kilimo hiki katika harakati za umwagiliaji na kufanya mazao yako yawe yenye afya na bora wakati wote
Fanya tafiti ya udongo uliopo eneo husika, Tafiti hii itakusaidia kujua udongo huo unafaa kwa mazao yapi, kwa mfano udongo wa kichanga hufaa sana kwa mazao ya mizizi hasa karanga na viazi vitamu nafikiri hata mihogo, hivyo huwezi kupanda karanga kwenye udongo wa mfinyanzi
Fanya tafiti ya mazao adimu sokoni, Hapa naelezea uhitaji wa mazao, huwezi kulima kilimo ambacho hakina uhitaji mkubwa sokoni, kwa mfano unaishi katika jamii ya wasukuma na kila kaya 10, 9 ni wasukuma tena wafugaji hapa huwezi kuanzisha biashara ya kuuza maziwa katika eneo hilo, nategemea utaanzisha duka la dawa za mifugo, kwa mfano huu natarajia umenielewa vyema
#stayhomestaysafe
Comments
Post a Comment