MASAL MASAL NA HISTORIA YAKE

           Masal Masal alizaliwa mnamo 14/02 /1994 huko mkoani Tabora katika jamii ya wafugaji (wasukuma) na ndiye mwanzilishi wa blog ya hii ya kilimo na ufugaji,
        Alianza safari ya Elimu yake mnamo mwaka 2005 Mpango Wa Elimu ya Msingi Kwa wale Walioikosa(MEMKWA) na mwaka uliofuata alifanya mtihani wa taifa Darasa la nne na alifaulu vizuri hivyo akaruhusiwa kuingia darasa la Tano na kuhitimu elimu ya msingi 2009
       Mnamo 2010 alibahatika kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Ilemba iliyopo katika kata ya Ilemba wilayani Sumbawanga mkoa wa Rukwa
   Mwaka 2013 alistahili kuhitimu kidato cha nne lakini haikuwa bahati kwake kwani aliugua wiki moja kabla ya mtihani na kupeleka kushindwa kufanya mtihani, kwa kuwa alikuwa ni mtu mwenye kupenda shule, alitamani afike mbali kimasomo, alijilazimisha kufanya mtihani ilhali alikuwa na hali mbaya
        Alifanikiwa kufanya masomo manne lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi hivyo akapelekwa ktk hospitali ya Misheni ya Kristo Mfalme alilazwa kama anavyosimulia
         "Nililazwa hospitali ya misheni ya Kristo Mfalme iliyopo katika manispaa ya Sumbawanga takribani wiki 3 au nne na kufunguliwa file namba 015368 la mwaka 2013"
        Safari yake ya elimu haikuishia hapo, anasimulia "Head master wangu aitwae CHUNGUEN MALATA alituma barua Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) ikieleza hali iliyonikumba na kuwaomba kama itawezekana nifanye mtihani mwaka unaofuata na kwa bahati nzuri nilikubaliwa kufanya mtihani"
Baada ya kukubaliwa kufanya mtihani anasema mambo hayakuishia hapo anaeleza changamoto iliyomkumba, huyu hapa
     
"Nilipigiwa simu na mkuu wa Shule na kuniambia kuwa nahitajika shuleni, ilikuwa mwezi Februari, baada ya kurudi shule nikaambiwa natakiwa kulipia pesa ya mtihani, nakumbuka ilikuwa Tshs50, 000/=
Ikabidi niwaeleze nyumbani lakini hawakunielewa si unajua jamii ya wafugaji?
Hapo nilikata tamaa na kuamua kuacha kabisa shule
  
     Nikaamua kujifunza kunyoa na nikaomba kazi ya kunyoa kwa rafiki yangu alikuwa na salon kipindi hicho anaitwa NDAKI SAID NG'HWAGI, nilifanya kazi lakini nikaona hailipi nikaamua kuondoka na kwenda mbali na kijiji cha Ilemba, miezi ilisogea na ilipofika Septemba mwishoni nikatamani kurudi shule
Niliamua kurudi shule na nikalipia pesa ya mtihani, ilikuwa imefikia Tshs85,000/=
Huwezi amini nilikuwa sijasoma chochote, kumbuka nyuma niliamua kuachana kabisa na masuala ya shule"
   Alifanyaje wakati alikuwa hajasoma chochote toka Februari?huyu hapa anasimulia "nilikuwa sina daftari hata moja nilichofanya nilikuwa namfuata mwanafunzi ninaeamini anamwandiko mzuri na notice nzuri nakusimama nyuma yake anaposoma na mimi ndo nakuwa nasoma anaposoma, na ilibidi niendane na kasi yake ya usomaji, wakati huo nyumbani hawajui niko wapi maana nilitoroka baada ya wao kushindwa kunilipia pesa ya mtihani na niliporudi shule kufanya mtihani nilifikia shuleni(hostel)
  
    Mwisho mtihani ulifika nikafanya na baadaye matokeo yakatoka na nikavuna nilichopanda, nilipata 1.1GPA sikwenda kokote na mwaka 2016 Julai nikaamua nijisajili kufanya mtihani wa kidato cha sita
Kwa bahati mbaya sikupata kabisa muda wa kujisomea kutokana na hali ngumu ya maisha, muda wote nilikuwa busy kutafta pesa ya chumba nilichopanga pamoja na pesa ya kununulia chakula,
   
    Siku ya mtihani ikawadia nikaenda kufanya na nikawa na III-17, Niliumia sana kwa maana kuwa ningelikuwa na mda mzuri wa kujisomea ningelikuwa na matokeo mazuri zaidi"
     Naamua kumuuliza kwani nyumbani ulikuwa ukiishi na akina nani? Anajibu
"Nyumbani nilikuwa nikiishi na mama yangu pamoja na kaka zangu, Baba alifariki(R. I. P) nikiwa mdogo sana hata simfahamu, mwenyezi Mungu ameuweka mahali panapostahili"
Vipi Baba hakuwa na ndugu zake labda wakakupiga jeki?
"Unajua mzee kipindi anaumwa alikuwa akiwasihi ndugu zake Kuwa siku akifariki, alitaka watoto wake waende kwa Baba mkwe(yaani kwa Babu mzaa mama) hivyo Alipofariki tukaletwa Sumbawanga kwa Babu

Hivyo Baba alikuwa na kaka zake ambao ni baba zangu wakubwa(nawaheshimu)toka mzee afariki alikuja mmoja mwaka 2007 kutujulia hali na, sijawahi kuomba msaada kwao"
      Walilichukuliaje agizo la Mzee wako kuhusu ninyi kwenda kuishi kwa Babu mzaa mama?
"sijajua walichukuliaje lakini nafikiri walilichulia kwa uzuri ndio maana mauti yalipomfika mzee walituruhusu kuondoka"
       Asante sana bwana Masal Masal kwa ushirikiano wako tunakutakia majukumu mema na kwa kheri

Comments

Popular posts from this blog

DHANA YA KAMUSI

CARROT CULTIVATION

SUNFLOWERS